Total Pageviews

Thursday, 26 November 2015


ELECTRONICS MONEY ( Tigo pesa, Mpesa, Airtell money)

Je wajua umuhimu wa kuanzisha au kutoa huduma ya electronics money, huduma ya kibenk kwenye simu yako. Hapa tutakujuza faida na hasara za electronics money kwa yule ambaye tayari anatoa huduma hiyo na kwa yule aliyepanga kuanza kutoa huduma kama hiyo kwa watanzania.

FAIDA ( ADVANTAGES)
  • kuongeza kipato (profit) kwa kupitia commission kutoka kwa makampuni ya simu kwa kutokana na jinsi unavyotoa huduma kwa wateja, uwingi wa wateja na kiwango kikubwa cha utoaji au uwekaji ndivyo upatavyo faida zaidi.
  • kuongeza marafiki hasa wateja zako ambao wengi wao hupelekea kuwa marafiki zako na kukufanya ujue au ujifunze mengi kutoka kwao.
  • kukufanya uwe bussy kama hukuwa na kitu cha kufanya, hii husaidia hasa wale vijana au watu wanaopenda kujiajili wenyewe.
  • kuzungusha pesa yako badala ya kuiweka tu bank au kwenye simu, utakuwa unaizungusha na kukuongezea kipato kila mwisho wa mwezi.
HASARA (DISADVANTAGES)
  • Ukiwa na mzunguko mdogo wa pesa na faida yake ni ndogo pia, hii inamaana hutapata faida kubwa bali utakuwa unaishia kulipia kodi tu ya pango na nauli ya kwenda na kuludi kwako kama unaishi mbali na kwenye biashara yako.
  • Umakini wa kuhesabu pesa wakati wa kutoa pesa kwa mteja na pia uandikaji wa number wakati wa kutuma kiasi kwenye simu ya mteja as kama ukikosea basi utakuwa umeingia hasara.
  • Kama utakuwa umeajiri mtu uwe makini na kumfahamu vizuri huyo mfanyakazi wako kwani udanganyifu au wizi wa pesa uko mwingi sababu huyu uliyemuajiri atakuwa anashika kiasi cha pesa kwa muda mwingi, therefore kama si mwaminifu itakuwa rahisi kukuibia au kukudanganya.
Angalizo
  •  Wateja wengine huleta pesa bandia( fake money) ili kupata zilizo halali kutoka kwako.
  • kumbuka si wateja wote huja kwa nia njema, as wengine hutaka kujua watoa au una kiasi gani kwenye account yako na pia cash mkononi ili wakuibie.
Hazo ni baadhi tu za maelezo ya faida na hasara za electronics money yaani tigo pesa, mpesa na aitell money.

No comments:

Post a Comment